‏ Psalms 7

Sala Ya Mtu Anayedhulumiwa

Ombolezo la Daudi kwa Bwana kwa sababu ya Kushi, Mbenyamini.

1 aEe Bwana, Mungu wangu, ninakukimbilia wewe,
uniokoe na kunikomboa na wote wanaonifuatia,
2 bla sivyo watanirarua kama simba
na kunichana vipande vipande, asiwepo wa kuniokoa.

3 cEe Bwana, Mungu wangu, kama nimetenda haya
na kuna hatia mikononi mwangu,
4 dau ikiwa nimemtenda uovu aliye na amani nami,
au nimemnyangʼanya adui yangu pasipo sababu,
5 ebasi adui anifuatie na kunipata,
auponde uhai wangu ardhini
na kunilaza mavumbini.

6 fAmka kwa hasira yako, Ee Bwana,
inuka dhidi ya ghadhabu ya adui zangu.
Amka, Mungu wangu, uamue haki.
7 gKusanyiko la watu na likuzunguke.
Watawale kutoka juu.
8 h Bwana na awahukumu kabila za watu.
Nihukumu Ee Bwana,
kwa kadiri ya haki yangu,
kwa kadiri ya uadilifu wangu,
Ewe Uliye Juu Sana.
9 iEe Mungu mwenye haki,
uchunguzaye mawazo na mioyo,
komesha ghasia za waovu
na ufanye wenye haki waishi kwa amani.

10 jNgao langu ni Mungu Aliye Juu Sana,
awaokoaye wanyofu wa moyo.
11 kMungu ni mwamuzi mwenye haki,
Mungu aghadhibikaye kila siku.
12 lKama hakutuhurumia,
atanoa upanga wake,
ataupinda na kuufunga uzi upinde wake.
13 mAmeandaa silaha zake kali,
ameweka tayari mishale yake ya moto.

14 nYeye aliye na mimba ya uovu
na achukuaye mimba ya ghasia huzaa uongo.
15 oYeye achimbaye shimo na kulifukua
hutumbukia katika shimo alilochimba mwenyewe.
16 pGhasia azianzishazo humrudia mwenyewe,
ukatili wake humrudia kichwani.

17 qNitamshukuru Bwana kwa ajili ya haki yake,
na nitaliimbia sifa jina la Bwana Aliye Juu Sana.
Copyright information for SwhNEN