‏ Psalms 97

Mungu Mtawala Mkuu

1 a Bwana anatawala, nchi na ifurahi,
visiwa vyote vishangilie.

2 bMawingu na giza nene vinamzunguka,
haki na hukumu ndio msingi wa kiti chake cha enzi.
3 cMoto hutangulia mbele zake
na huteketeza adui zake pande zote.
4 dUmeme wake wa radi humulika dunia,
nchi huona na kutetemeka.
5 eMilima huyeyuka kama nta mbele za Bwana,
mbele za Bwana wa dunia yote.
6 fMbingu zinatangaza haki yake,
na mataifa yote huona utukufu wake.

7 gWote waabuduo sanamu waaibishwa,
wale wajisifiao sanamu:
mwabuduni yeye, enyi miungu yote!

8 hSayuni husikia na kushangilia,
vijiji vya Yuda vinafurahi
kwa sababu ya hukumu zako, Ee Bwana.
9 iKwa kuwa wewe, Ee Bwana, ndiwe Uliye Juu Sana kuliko dunia yote;
umetukuka sana juu ya miungu yote.

10 jWale wanaompenda Bwana na wauchukie uovu,
kwa maana yeye hulinda maisha ya waaminifu wake
na kuwaokoa kutoka mkononi mwa mwovu.
11 kNuru huangaza wenye haki
na furaha kwa watu wanyofu wa moyo.
12 lFurahini katika Bwana, ninyi mlio wenye haki,
lisifuni jina lake takatifu.
Copyright information for SwhNEN